STADI ZA MAISHA:
Sura Madhumuni
Utangulizi wa
Stadi za
Maisha
Orodhesha tabia hatarishi wanazokutana nazo vijana katika jamii
Tambulisha stadi za maisha ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kupunguza
hatari na kujenga maisha ya kiafya ya baadae
Orodhesha aina nne za stadi za maisha
2
Stadi za Hisia
Kuelewa maana ya misamiati ya kujiheshimu na kujiamini
Kuoanisha kiwango cha mtu cha kujiheshimu
Kufikiri jinsi ya kuboresha afya ya kihisia ya mtu binafsi
3
Stadi za
Mawasiliano
Tambua umuhimu wa mawasiliano ya vitendo
Elewa mawasiliano ya tabia za ugomvi, utulivu na msimamo
Elewa na fanya mazoezi ya kufuata hatua za kufanya mwitiko wa tabia ya
msimamo
Tambua mbinu za kushawishi na namna ya kukabiliana nazo
4
Kufanya
Maamuzi
Tambua umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi
Eleza hatua zinazotumika kufanya maamuzi sahihi
5
Mapenzi na
Mahusiano
Elewa umuhimu wa urafiki
Tambua shinikizo rika na fikiria jinsi mtu anavyoweza kupambana nao
Fikiria kuhusu mapenzi na umuhimu katika uhusiano wa kimapenzi
6
Ngono ya
Kulazimishwa
Kubainisha kwamba ngono ya kulazimishwa hutokea na ni hatari
Kugundua hali ambazo ngono ya kulazimishwa inaweza kutokea
Fikiria kuhusu njia ambazo mtu anaweza kujikinga mwenyewe
7
Majukumu ya
Kijinsia
Kueleza maana ya “majukumu ya kijinsia”
Kueleza tofauti kati ya “jinsi” na “majukumu ya kijinsia”
Kuorodhesha majukumu yanayotarajiwa kwa wanaume na wanawake katika
jamii
Kueleza changamoto kwa majukumu ya sasa ya kijinsia na jinsi
yanavyoweza kubadilishwa katika hii jamii
8
Ndoto na
Malengo
Kufikiria kuhusu malengo na tamaa zao
Kugundua kwamba kupanga na kufanya vitendo kunahitajika kufanya ndoto
na malengo kutokea
Wenye Elimu Ndogo
Kila kikundi cha vijana ni tofauti. Ni muhimu muwezeshaji achukue muda wa
kutathmini mahitaji ya kikundi ili njia bora zinazofaa za kukidhi mahitaji hayo ziweze
kutumiwa. Ili kutumia mazoezi yaliyo kwenye kitabu hiki kwa ajili ya vijana wenye
uzoefu mdogo wa kusoma na kuandika, fuata kanuni na mwongozo hapo chini.
Kanuni za Msing
:
Kuwa mbunifu: unaweza kutafuta njia za kuchekesha na za kuvutia ili kutekeleza
zoezi hilo hilo au zoezi jipya kabisa kufanikisha malengo.
Shirikisha kikundi:
Washirikishe washiriki mara nyingi iwezekanavyo kukusaidia
katika maandalizi yoyote yanayohitaji kufanyika, pamoja na kutayarisha chumba,
kuandaa zana za kazi n.k.
UTANGULIZI
Mwongozo wa Stadi za Mpango wa Maisha Tanzania 9
Tumia vielelezo vya kuona na kusikisia
kadri iwezekanavyo. Hii ni pamoja na
mabango, picha, michoro, mifano na zana nyingine za kienyeji zitakazotajwa na
kikundi n.k.
Miongozo:
_ Tumia lugha rahisi na ya wenyeji pamoja na istilahi rahisi zinazojulikana kadri
iwezekanavyo.
_ Tumia kazi za vikundi na kuwashirikisha zaidi.
_ Waache wanakikundi wajibu maswali na watoe muhtasari kadri iwezekanavyo
kwa kutumia lugha zao za makabila na istilahi zao.
_ Tumia mifano halisi ya maisha unapojaribu kutoa hoja ya kweli.
_ Tumia vitu vya kawaida na vya kila siku kama sehemu ya nyenzo za
kufundishia pale inapowezekana kwa mfano, karatasi, makopo, vifungo, vijiti
n.k. Hakikisha kikundi kinakusanya vitu hivi pindi vikihitajika.
_ Mwulize mtu mmoja katika kikundi arudie au anakili kile ulichosema au
ulichofanya ili kuhakikisha kwamba kikundi kinaelewa.
_ Tumia vitendo vitakavyowashirikisha vijana kama vile:
· Kucheza michezo; michezo ya karata ni mizuri. Hii inaweza kuhitaji
kutayarishwa kuanzia mwanzo kabisa kutegemeana na jambo lenyewe.
Achia kikundi kisaidie kama inawezekana, kwa kuwaruhusu:
o kiainishe zoezi
o kikusanye na kukata picha
o kikate au kubandika kadi
· Kutengeneza vigandisho (picha zitengenezwazo kwa kukata vipande
vidogo vya karatasi na kuvibandika kwenye mbao au kiegemeo chochote
kigumu).
· Kutunga nyimbo na mashairi kwa kutumia taarifa za kweli. Hii inasaidia
kuzikumbuka taarifa za kweli kirahisi, hasa kama washiriki watakuwa
wametunga nyimbo zao wenyewe na mashairi yao na kukifundisha
kikundi.
_ Wahimize na kuwaruhusu wanakikundi kuchangia uzoefu wao ili waweze
kujifunza kutoka kwa kila mtu.
_ Tumia sanaa ya jadi, hadithi na methali zinazohusiana na uzoefu wa maisha ya
kujenga maadili, kufundisha na kujifunza.
_ Wahimize kwa mifano ya maonyesho pale inapowezekana. Uongozwe na
mahitaji ya kikundi.